Timu ya taifa ya Ujerumani jana imeibuka kidedea kwa kuichapa Chile goli 1-0 kwenye mechi ya fainali ya kombe la mabara nchini Urusi.
Goli la Ujerumani lilipatikana dakika 20 za kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wa klabu ya BorussiaDortmund, Larsi Stindl goli ambalo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo.
Hiyo ni kwa mara ya kwanza kwa Ujerumani wa kutwa kombe hilo ambalo ndiyo linaanza kabla ya kombe la dunia.
Kabla ya mchezo huo kulikuwa na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Mexico na Ureno ambapo Ureno iliibuka kidedea kwa kuilaza Mexico goli 2-1, magoli ya Ureno yakifungwa na Pepe na Adrien Silva huku goli la Mexico likifungwa na Luis Neto