Maofisa wa Polisi nchini Ujerumani wamesema kuwa shambulizi lililotokea uliotokea kwenye gari la Borussia Dortmund halikuwa la kigaidi.

Gari hilo liliwabeba wachezaji wa Borussia Dortmund kuelekea katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya lililengwa na milipuko mitatu.

Polisi hao wamesema kuwa barua ilikutwa pembezoni mwa eneo la shambulizi hilo lakini haikuwa na maelezo ya kutosha.

Mchezaji mmoja wa Dortmund na raia wa Uhispania Marc Bartra amejeruhiwa na kufanyiwa upasuaji.

Taarifa za kiintelijensia zinasema kuwa zinachunguza shambulizi hilo kama linahusika na mashabiki wa timu ya upinzani.

Mchezo kati ya Dortmund na Monaco umeahirishwa ambapo utachezwa leo katika uwajan wa Sydney Iduna Park.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *