Wakala wa Majengo nchini (TBA) umesema unatarajia kuanza ujenzi wa nyumba za kisasa katika eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam Septemba 29 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Elius Mwakalinga amesema kuwa tayari serikali imewapa Sh bilioni tano, kwa ajili ya kuanza ujenzi huo.

amesema kuwa baada ya Rais, kuwataka TBA kuanza ujenzi huo mara moja, na kwamba tangu Septemba 20 mwaka huu, ulianza kwa hatua za mwanzo ikiwa ni pamoja kuandaa michoro na kurejesha mipaka ya eneo hilo ambayo itasaidia katika kupanga nyumba zinazotarajiwa kujengwa.

Aidha alisema kuanza kwa ujenzi huu kunatarajia kutengeneza ajira zaidi ya 600 kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa siku moja.

Ameongeza kuwa ujenzi huo, utakuwa na nyumba tano zenye ghorofa nane kila moja ambazo zitawaweka wakazi 644 waliobomolewa nyumba zao mwaka 2011, majengo mawili ya ofisi pamoja na majengo ya biashara.

Aidha, alisema nyumba hizo hazitawanufaisha wale waliobomolewa nyumba zao pekee bali hata wananchi wengine wanaweza kunufaika na nyumba hizo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *