Serikali imesema kuwa ujenzi wa daraja refu kuliko yote nchini la Salender unatarajia kuanza juni mwakani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema hayo jana baada ya mazungumzo na balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum- Young Ikulu jijini Dar esa Salaam.

Rais Magufuli amesema wamepata fedha kutoka benki ya Exim ya nchini Korea.

Aliyekuwa waziri wa fedha wa serikali ya awamu ya nne Saada Mkuya alisaini hati ya mkataba wa makubaliano ya mkopo wa Dola 91 milioni za Marekani sawa na zaidi ya sh196 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo septemba mwaka jana.

Rais Magufuli amesema mchakato wa kulijenga daraja hilo litakalounganisha ufukwe wa Coco na Aga Khan kupitia baaharini nuaendelea vizuri na sasa kampuni inayofanya usanifu kutoka korea ipo kwenye hatua za mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *