Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya gari la mizigo kuvamia kundi la waenda kwa miguu, karibu na msikiti ulioko kaskazini ya mji mkuu wa Uingereza London.

Polisi wamelielezea tukio hilo kama ni ajali kubwa, Tayari mtu moja amekamatwa kufuatia shambulio hilo lililotokea katika wilaya ya Finsbury Park.

Baraza Kuu la Waislamu nchini Uingereza limesema kuwa walengwa wa tukio hilo walikuwa ni waumini, huku majeruhi wengi wakiaminika kuwa ni wale waliokuwa wamemaliza tu kuswali swala ya jioni baada ya kuumaliza mfungo wa siku wa Ramadhan.

Video zilizotumwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha watu walio katika taharuki, kuhu wakijaribu kuwasaidia majeruhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *