Winga wa Manchester United, Adnan Januzaj amejiunga na klabu ya sunderland kwa mkopo.

Uhamisho huo umemuunganisha na meneja wake wa zamani, David Moyes pamoja na wachezaji wenzake wa Manchester United, Donald Love na Paddy McNair waliyejiunga na timu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 5.5 wiki hii.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ubeligiji alikuwa anataka kuondoka Old Trafford moja kwa moja lakini klabu hiyo ya United iliamua kumtoa kwa mkopo.

Kitchee FC v Manchester United

Januzaj amefunga magoli matano katika mechi 63 alizocheza kwenye klabu ya United.

Mkataba wake na Manchester United utamalizika mwaka 2018.

Winga huyo alijiunga na timu ya Borussia Dortmund msimu uliopita kwa mkopo wa miezi minne, lakini alicheza mechi 12 kabla ya kurudi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *