Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema hana tatizo lolote na golikipa namba moja wa timu hiyo Joe Hart baada ya kumuweka nje kwenye mechi ya kwanza ya ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Sunderland.

Kocha huyo aliamua kumuweka nje Joe Hart na kumuanzisha golikipa, Willy Caballero kwenye mechi dhidi ya Sunderland iliyofanyika katika uwanja wa Etihad ambapo City walishinda 2-1.

hart

Guardiola amesema Hart ni golikipa mzuri sana ila kwenye mechi dhidi ya Sunderland aliamua kumpanga Willy Caballero kwani naye pia ana uwezo mzuri wa kudaka, kwa hiyo watu wasifikirie vibaya kama ana ugomvi na Hart.

Vile vile Guadiola ameongeza kwa kusema kwamba kwasasa ana kikosi kipana kwa hiyo atachagua yeye nani aanze kwenye kikosi cha kwanza na nani asianze ila wachezaji wake wote wanauwezo sawa.

Manchester City walifanikiwa kushinda mechi yao ya kwanza ya ligi kuu nchini Uingereza chini ya Guardiola baada ya kushinda 2-1 kufuatia goli la penati la Sergio Aguero na goli la kujifunga la McNair huku goli la Sunderland likifungwa na Jermain Defoe.

Joe_Hart

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *