Uholanzi imemtimua kocha wa timu yake ya taifa Danny Blind baada ya kuifundisha kwa takriban miaka miwili.

Hii inafuatia kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya Bulgaria siku ya Jumamosi na kuwaacha Uholanzi katika nafasi ya nne kwenye mbio za kufuzu kushiriki kombe la dunia.

Blind mwenye miaka 55 alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Guus Hiddink mwaka 2015 huku ikishuhudiwa kikosi chake kikishindwa kufuzu fainali za michuano ya Ulaya mwaka jana.

Chama cha soka nchini Uholanzi kimesema kuwa ameicha timu hiyo katika wakati mgumu kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Urusi.

Fred Grim ameteuliwa kuwa kocha wa mpito na atakiongoza kikosi hicho siku ya Jumanne dhidi ya Ufaransa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *