Staa wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameanza kufanya mazoezi mepesi na klabu yake baada ya kupona majeraha ya goti.

Ronaldo aliumia goti wakati akiitumikia timu yake ya taifa katika mechi ya fainali ya kombe la Euro dhidi ya Ufaransa ambapo Ureno ilitwaa ubingwa huo baada ya kushinda 1-0 kwenye fainali hiyo.

Staa huyo alikaa nje ya uwanja toka kumalizika kwa fainali hiyo na kupelekea kukosa mechi za timu yake ya Real Madrid za kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini Uhispania pamoja na mashindano mengine.

Ronaldo kwasasa ameanza kufanya mazoezi na timu yake hiyo kwaajili ya msimu mpya wa ligi kuu nchini Uhispania ambao unatarajiwa kuanza mwezi huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *