Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amepasuka uso baada kupigwa ngumi wakati akigombelezea ugomvi usiomuhusu.

Shamsa amedai kuwa alipigwa ngumi ya uso katika harakati za kutafuta usalama wa watu hao ambao walikuwa wakipigana na yeye akaamua kwenda kugombelezea.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Shamsa ameandika kuhusu mkasa huo huku akiambatanisha na picha ambayo amepasuka uso.

Aliandika kama ifuatavyo, Mimi ngumi..HUYU mtu alishiba sana aiseee ngumi ilikuwa nzito sana.. niombeeni ndugu zangu panauma,” aliandika Shamsa Instagram. Kwa sasa muigizaji anaendelea na matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *