Uganda: Familia yamteuwa Zari kusimamia mali za Ivan Don

0
831

Familia ya Ivan Don aliyekuwa mume wa Zari imemteuwa Zari kuwa msimamia wa mali za Ivan zikiwemo shule na vyuo zilizopo nchini Afrika Kusini.

Mwanamama huyu ataanza kazi rasmi ya kusimamia na kuendeleleza vyuo na shule zilizoachwa na Ivan baada ya maziko siku ya Jumanne nchini Uganda.

Kaka wa Ivan na aliekuwa mtu wa karibu yake Pinto amesema hayo wakati wa kuaga mwili wa marehemu Ivan katika Kanisa nchini Uganda.

Pinto amesema tatizo la moyo ni ugonjwa uliopo kwenye familia yao na kitendo cha Zari kuwa na watoto 3 wa Ivan tayari amequalify kuwa msimamizi wa mali hizo kwa ajili ya future ya watoto ikizingatiwa wazazi wote wawili wa IVAN walishafariki.

Zari akiwa kanisani na watoto wake wakati wa kuaga mwili wa Ivan Don nchini Uganda.
Zari akiwa kanisani na watoto wake wakati wa kuaga mwili wa Ivan Don nchini Uganda.

Pinto amekanusha habari zinazombaa kwamba wana ndugu wanagombania mali huku akisema pesa kwenye familia yao sio tatizo ni kitu kipo kwenye blood.

Ivan Don amefariki dunia nchini Afrika Kusini alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo na anatarajiwa kuzikwa leo nchini Uganda.

Ivan amefanikiwa kupata watoto watatu na mwanadada Zari kabla ya kuachana na kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na Diamond Platnumz.

LEAVE A REPLY