Serikali ya Uganda imethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya ndege katika maeneo karibu na fuo za Ziwa Victoria.

Virusi hivyo vimegunduliwa kwa ndege wa porini wanaohama hama, bata wanaofugwa na kuku.

Wakuu nchini humo sasa wametoa tahadhari kwa jamii za maeneo hayo kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hausambai na kuwaambukiza watu.

Wakazi wa maeneo hayo, wamesema kuwa, walipata mizoga ya ndege wengi waliokuwa wakihamia Uganda wakati wa majira ya baridi kutoka maeneo ya kaskazini mwa dunia.

Uchunguzi uliofanywa na wataalamu, yalithibitisha kuwa ndege hao walifariki kutokana na maradhi ya Highly Pathogenic Avian Influenza au bird flu, yaani homa kali ya ndege kama inavyofahamika.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *