Klabu ya Leicester city wameibuka na ushindi wa pili katika michuano ya ulaya kwa kuichapa FC Porto kwa bao 1-0 katika nuwanja wa King Power.

Real madrid imelazimshwa 2-2 dhidi ya Borrusia Dortmund kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa Sgnal Iduna Park huku Monaco wakavutwa shati nyumbani kwa sare ya bao 1-1 na Bayer Leverkusen.

Sporting Lisbon wakiwa nyumbani wamewalaza Legia Warszawa toka Poland kwa mabao 2-0 huku FC Copenhagen wameibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Club Brugge.

Juventus wameibuka na ushindi ugenini kwa kuichapa Dinamo Zagreb mabao 4-0 na Sevilla wameshinda 1-0 dhidi ya Lyon huku Tottenham ikichomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji CSKA Moscow.

Mechi nyingine za klabu bingwa barani Ulaya zianatarajiwa kuchezwa leo katika viwanja tofauti Barani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *