Michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya katika msimu huu wa mwaka 2016/17 imeendelea usiku wa kuamkia leo kwa takribani makundi manne kuingia dimbani.

Arsenal ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani ilipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Basel ya nchini uswizi, magoli yote yalifungwa na Theo Walcott.

PSG ikiwa ugenini ilipata ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria.

Besiktas imeenda sare ya 1-1 dhidi ya Dynamo Kyiv. Huku SSC Napoli ikiibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Benfica.

Borussia Monchengladbach ikiwa nyumabi imekubali kichapo cha 2-1 dhidi ya Barcelona. Na mchezo kati ya Celtic na Manchester City walitoka sare ya 3-3.

Atletico Madrid nayo ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Bayern Munich. Na FC Rostov ikiwa nyumbani ilitoka sare ya 2-2 dhidi ya PSV Eindhoven.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *