Mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA)  imetangza kumfikisha mahakani mkurugenzi mtendaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi (UDART), David Mgwasa kwa kile ilichoeleza kutoza nauli kubwa zaidi ya iliyokubaliwa.

Mkurugenzi wa SUMATRA, Gilliard Mgewe aliwaaambia waandishi wa habari kuwa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa abiria wakidai kutozwa nauli kubwa kuliko iliyoelekezwa hapo awali, walifanya uchunguzi na kubaini kuwepo na vitendo hivyo.

Mgewe amesema inapaswa anaetoka Mbezi Luis kulipia shilingi 400 hadi Kimara na kulipia shilingi 400 nyingine anapofika Kimara na kutaka kuendelea na safari yake, Udart imekuwa ikmtoza abiria huyo jumla ya shilingi 1,050 (400 +650) badala ya jumla ya shilingi 800.

Mkurugenzi huyo wa SUMATRA pia amesema wamepanga kuwafikisha mahakamani madereva wa mabasi ya mwendokasi wanaoendesha magari hayo kwa mwendo wa zaidi ya kiliometa 90 kwa saa badala ya kuwalipisha faini kama ilivyo hivi sasa.

Akijibu tuhuma hizo mkurugenzi wa UDART, Mgwasa amesema haogopi kupelekwa mahakamani kwa kile alichodai haiwezekani mtu alipe nauli hiyo hiyo kwa safari mbili tofauti.

Hata hivyo Mgwasa aliomba kupelekewa ushahidi wa tiketi unaothibitisha kuwepo kwa ulipishwaji wa nauli kinyume na bei elekezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *