Basi la Kampuni ya Usafirishaji ya UDA lenye namba za usajili T 696 CVP limegonga treni katika eneo la Kamata Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo  wakati basi hilo likotokea stendi ya Gerezani Kariakoo kuelekea Mbagala na kuua mtu mmoja huku wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa.

 

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu. Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *