Mshambuliaji wa Real Madridi, Cristiano Ronaldo ameivusha klabu yake hatua ya nusu fainali baada ya kushinda mabao matatu kwenye ushindi wa 4-2 dhidi ya Bayern Munich.

Mechi hiyo iliyomalizika 4-2 hata hivyo ilijaa utata na mshindi alipatikana katika muda wa ziada.

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Arturo Vidal alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu kiungo wa Real Madrid Assension.

Bayern, ambao walihitaji mabao mawili kusonga, alikuwa wameongoza kupitia penalti iliyofungwa na Robert Lewandowski.

Madrid walitatizika kutamba kwenye mechi hiyo iliyochezwa Bernabeu kabla ya Ronaldo kufunga kwa kichwa kutokana na krosi ya Casemiro.

Bayern walijibu sekunde 36 baadaye Sergio Ramos alipojifunga na kulazimisha mechi hiyo kuingia muda wa ziada.

Kwa upande wa Atletico Madrid walisonga kwa kuwaondoa Leicester City baada ya kutoka 1-1 kwenye mechi ya jana.

Kwenye robofainali hizo nyingine, Barcelona wanakutana na Juventus nao Monaco watakutana na Borussia Dortmund.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *