Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa uchunguzi wa watoto pacha ambapo mmoja anadaiwa kuibiwa katika hospitali ya Temeke imebainika kuwa mama huyo Asma Juma alikuwa na mtoto mmoja.

Akitoa ufafanuzi wa kuhusu uchunguzi huo, mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Waziri Ummy, Profesa Charles Majinge amesema kuwa kunawezekana kuna makosa yamefanyika katika vipimo vya utrasaund.

Pia amesema kuwa wataalamu wa Hospitali ya Temeke wamefanya makosa kumfanyia upasuaji bila kumfanyi vipimo zaidi vya utrasaound.

Profesa Majinge amesema kuwa hapakuwa na sababu ya mama huyo, Asma Juma kuandikiwa kufanyiwa upasuaji wa dharura ingawa hakufanyiwa huduma hiyo.

Kabla ya kukutana na waandishi wa habari, waziri Ummy na Profesa Majinge wamekutana na mzazi huyo Asma Juma pamoja na familia yake na kumuambia habari za uchunguzi huo na kusababisha mama huyo kuangua kilio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *