Uchunguzi wa madai ya nyota wa Hollywood, Brad Pitt kuhusu tabia ya ukatili dhidi ya mwanawe wa kiume umesitishwa.

Maafisa wa huduma kwa jamii mjini Los Angeles wamekuwa wakichunguza madai kwamba Bw Pitt alimgonga Maddox, 15, wakiwa kwenye ndege ya kibinafsi.

Mkewe Angelina Jolie aliwasilisha ombi la talaka siku ambayo kisa hicho kilitokea.

Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya mwongo mmojja.

Bw Pitt sasa anapigania kupata haki sawa ya kukaa na watoto wao sita.

Msemaji wa Idara ya Huduma za Familia ya Watoto LA amesema idara hiyo haiwezi kuthibitisha iwapo maafisa wake walimchunguza itt.

Pitt na Jolie walianza mahusiano yao wakiandaa filamu ya 2005 kwa jina Mr & Mrs Smith, ambapo waliigiza wachumba walio kwenye uhusiano uliokwama. Walioana 2014.

Ndoa hiyo ilikuwa ya pili kwa Pitt baada yake kutaliniana na nyota mwigizaji wa kipindi cha Friends, Jennifer Aniston.

Jolie ilikuwa ya tatu baada ya ndoa zake kwa Billy Bob Thornton na Jonny Lee Miller.

Wana watoto sita Maddox, Pax, na Zahara, ambao ni wa kupangwa, na wa kuzaliwa Shiloh na pacha Knox na Vivienne.

Pitt na Jolie walifunga ndoa kwenye sherehe ya harusi ya faraghani eneo la Provence, Ufaransa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *