Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC uhenda ikaahirisha Uchaguzi ujao nchini humo baada ya kampuni ya Ufaransa ya Safran Morpho kuomba muda zaidi kuboresha mitambo inayotumiwa kuwatambua wapiga kura.

Mbali na hilo, Muungano wa Upinzani Nasa, unaoongozwa na Raila Odinga, umesema Uchaguzi hautafanyika iwapo marekebisho hayatafanyika ndani ya Tume ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa Ezra Chiloba Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo.

Chama cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta kinashutumu shinikizo hilo la upinzani na kusisitiza uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa.

Uchaguzi wa Kenya unarudiwa baada ya matokeo ya awali yaliyompa ushindi Rais Kenyatta kutenguliwa na mahakama kuu nchini humo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *