Kiongozi wa tume ya Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Maman Sidikou amesema nchi hiyo huenda isiandae uchaguzi wa rais uliotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Akiongea leo jijini Kinshasa,Maman Sidikou amesema kwamba ni raia wenyewe wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ndiyo watakaoamua lini uchaguzi huo ufanyike.

Kwa upande mwingine baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa wameonya kwamba kucheleweshwa kwa uchaguzi huo huenda kukazua vurugu nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *