Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umefungwa kwa muda baada ya mtu aliyekuwa na kisu kujaribu kumshambulia afisa wa usalama karibu na ubalozi siku hapo jana.

Lakini mtu huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na maofisa wa polisi nchini Kenya huku taarifa zinasema kuwa hakuna afisa yeyote wa ubalozi huo aliyeathiriwa na kisa hicho.

Taarifa kutoka ubalozi huo zinasema “Ubalozi utafungwa Oktoba 28 na huduma zote za kibalozi zimesitishwa, lakini huduma za kibalozi za dharura kwa raia wa Marekani zitaendelea kutolewa kama kawaida.

Maafisa wa ubalozi huo wametoa wito kwa raia na wafanyakazi wake kuwa makini kuhusu usalama wao.

Polisi nchini Kenya wanachunguza kubaini iwapo mt huyo aliyepigwa risasi alikuwa na washirika.

Maafisa watano wa idara ya uchunguzi wa jinai ya Marekani (FBI) walifika eneo la tukio muda mfupi baadaye pamoja na polisi wa Kenya kufanya uchunguzi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *