Rapa nyota wa Marekani, Michael Ray Stevenson ‘Tyga’ amesema kuwa amewahi kuonywa kutoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mwanamitindo Kylie Jenner.

Tyga amesema kuwa licha ya watu wake wa karibu kumuonya kuhusu msichana huyo lakini hakuambiwa sababu za kuwa mbali na mwanamke huyo hivyo akapotezea.

Tyga amesema yeye alikuwa na mapenzi ya dhati na mwanamke huyo lakini kila alipokutana na marafiki zake walimtahadharisha kuwa mbali naye jambo amblo hadi leo anajiuliza kwanini walimwambia vile.

Tyga aliongeza kwa kusema kuwa marafiki zake wengi walikuwa wakimtahadharisha kuwa mbali na Kylie bila kumpa sababu lakini alishindwa kuwasikiliza kwani moyoni alimpenda sana.

Kylie ambaye ni ndugu na Kim Kardashian yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na rapa huyo wa Marekani ambapo uhusiano wao ndiyo zidi unapamba moto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *