Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu amekamatwa na Jeshi la Polisi leo asubuhi katika maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam.

Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema alikwenda mahakamani hapo kusikiliza kesi yake nyingine ya uchochezi ndipo alipokamatwa na jeshi la polisi.

Ofisa Habari wa Chadema Tumaini Makene amethibitishwa kukamatwa kwa Mbunge huy.

 Makene amesema kuwa “Ni kweli Tundu Lissu amekamatwa alipokuwa akitoka mahakamani kusikiliza kesi yake. Polisi hawajaeleza kwa nini wamemkamata na mpaka tunavyoongea sasa yupo kwa Kamanda Simon Sirro, taarifa zaidi tutawajuza,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *