Tundu Lissu kufanyiwa upasuaji mwingine

0
281

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu leo anatarajjiwankufanyiwa oparesheni nyingine ya mguu wake wa kulia ambao bado una matatizo kutokana na risasi alizopigwa.

Upasuaji huu utakuwa ni wa 20 tangu alipoanza kutibiwa, baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka jana.

Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji kwa matibabu amesema kwamba oparesheni hiyo ni sehemu ya tiba ya mguu huo huku akieleza kuwa kwenye mikono yuko salama kitabibu.

Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana mnamo Septemba 7 mwaka jana nyumbani kwake, Area D mkoani Dodoma.

LEAVE A REPLY