Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amekimbizwa hospitali mchana huu  baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchana akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa ametoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana.

Gari la Tundu Lissu likiwa na alama ya risasi
Gari la Tundu Lissu likiwa na alama ya risasi

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *