Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) amekamatwa na Polisi asubuhi ya leo nyumbani kwake mkoani Dodoma.

Lissu baada ya kukamatwa amepelekwa Ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani humo kwa ajili ya mahojiano.

Mbunge huyo anasafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufikishwa mahakamani mkoani humo.

Tundu Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa Cahdema anakabiliwa na madai ya kukiuka masharti ya dhamana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *