Baada ya mahakama ya wilaya ya Kilombero kumhukumu mbunge Peter Lijuakali kwenda jela miezi sita bila ya kulipa faini, Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu ameahidi kumsaidia mbunge huyo.

Tundu Lissu amesema kuwa hukumu aliyopewa Mbunge huyo ni ya kisiasa na ilipangwa na chama cha mapinduzi kwa ajili ya kuikomoa Chadema lakini atahakikisha anamtetea mbunge huyo mahakamani kwa kukata rufaa.

Peter Lijuakali: Mbunge wa Kilombero aliyehukumiwa miezi sita jela.
Peter Lijuakali: Mbunge wa Kilombero aliyehukumiwa miezi sita jela.

Mwanasheria huyo wa Chadema amesema hayo leo makao makuu ya chama Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati wa kikao na waandishi wa habari.

Lissu amesema Chadema inaamini Lijualikali ni mfungwa wa kisiasa na kwamba adhabu ya kifungo bila faini, ni kinyume na haki za binadamu na imetolewa kisiasa.

Pia Lissu amesema kuwa kisheria, hata kama mbunge huyo atatumikia kifungo hicho, hataweza kuvuliwa ubunge wake kwa sababu sheria inaeleza kuwa mtu atakayevuliwa ubunge, ni aliyetumikia kifungo cha zaidi ya miezi sita na kwamba kosa alilolifanya, siyo la utovu wa uaminifu kama katiba inavyoeleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *