Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amefunguka na kumchana Waziri Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuwa anahamasisha vijana kujiajiri wakati yeye analialia.

Lissu amesema hayo baada ya kuona video ya Waziri Mwijage akisema kuwa yeye anaipenda sana kazi yake ya Uwaziri na kusema watu ambao wamepewa viwanda wasitake kumponza akapoteza nafasi hiyo.

Baada ya kuona video hiyo Tundu Lissu amesema kuwa mawaziri mbalimbali wamekuwa vinara kuhubiri majukwani na kuwahamasisha vijana waliomaliza vyuo mbalimbali kwamba wanatakiwa kujiajiri wakati wao wenyewe wameshindwa kufanya hivyo.

Akiwa mkoani Tanga, Rais Magufuli amemsifu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa kuanzisha viwanda mbalimbali lakini amesema kuwa anachukizwa na Waziri huyo anapokuwa mzito kufanya maamuzi ya kupokonya viwanda mbalimbali ambavyo havifanyi kazi na kusema sasa anataka kusikia watu wakinyang’anywa viwanda hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *