Baada ya kusambaa kwa habari kupitia akaunti ya Twitter ikionesha Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akimpongeza Alikba kwa kuachia wimbo mpya na kuuponda wimbo kutoka WCB, mbunge huyo amekanusha taarifa hiyo.

Lissu ameikana akaunti ya Twitter iliyoandika maoni hayo ya kumpongeza Alikiba, huku ikiwa na picha ya wanamuziki wanaofanya kazi chini ya lebo wa Wasafi.

Lissu amesema hafahamu chochote kuhusu akaunti hiyo na maoni yaliyotolewa akitaka mwandishi amfafanulie.

Amesema kuwa “Wananisingizia tu, ni wimbo gani wa Alikiba?” akimaanisha haelewi chochote kinachoendelea kuhusu uwepo wa wimbo wa “Seduce Me.”

Pia amesema kuwa  “Hiyo akaunti ya Twitter si yangu na nilishasema tangu mwaka jana”

Jana akaunti hiyo ilikuwa gumzo kwenye mitandao ikiwa imebeba ujumbe unaosema: “Hakuna kitu kibaya kama wanaume sita kuvaa mawigi kupambana na mtu mmoja. #seduceme#.

Tweet hiyo iliambatanishwa na picha ya Kundi la Wasafi wakiwa wamevaa mawigi ambayo waliitoa sambamba na wimbo wao wa “Zilipendwa”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *