Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amekamatwa wakati akiwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Tundu Lissu amekamatwa na Mlinzi wa amani alipokuwa anatoka mahakamani Kisutu huku ikielezwa kuwa wamemkamata kwa ajili ya mahojiano.

Habari za kukamatwa kwa mbunge huyo zimethibitishwa na Afisa habari wa Chadema Tumaini Makene baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Tundu Lissu alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili mfanyabiashara Yericko Nyerere anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pia.

Afisa habari huyo amesema kuwa  wakati gari la Lissu likiwa getini tayari kwa kutoka, likazuiliwa na maofisa wa polisi mahakamani hapo.

Pia amesema kuwa nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na kutakiwa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police).

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *