Mwanamuziki wa Bongo fleva,  Tunda Man kutoka Tip Top Connection pamoja na mpenzi wake wa muda mrefu wamefanya ‘send-off’ wakijiandaa kuingia katika maisha ya ndoa.

Picha za sherehe hiyo zilsambaa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha Tunda Man pamoja na mpenzi wake wakiwa kwenye ‘send-off’.

Mmoja kati ya wasanii ambao walihudhuria shughuli hiyo ni Dojo Janja ambapo alimpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo.

Tunda Man anaungana na wasanii wenzake ambao wameingia maisha ya ndoa kama vile Mwana FA, H- Baba, Roma na wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *