Mwanamuziki wa Bongo fleva, Tunda Man amesema kuwa anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi ifikapo Novemba 12 mwaka huu.

Tunda amesema kuwa ndoa hiyo ilikuwa inafanyike miezi michache iliyopita lakini amedai kuna mambo yaliingilia na kuharibu mipango ya ndoa hiyo.

Mkali huyo wa nyimbo ya mama kijacho aliendela kusema kuwa “Kusema kweli suala la kuoa, naoa mwezi wa kumi na moja tarehe 12,” alisema Tunda “Kwa hiyo mtu yeyote anakaribishwa na nipo tayari kuingia kwenye maisha ya ndoa”.

Vile vile aliongeza kwa kusema “Kwa wale ambao hawajapata kadi wanione, unajua kuna watu mpaka waalikwe ndo wanaweza kuja,”.

Mwanamuziki huyo amesema anaimani akiingia kwenye ndoa kuna neema ambayo ataipata kutoka kwa mwenyezi mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *