Mkali wa nyimbo ya ‘Mama Kijacho’ Tunda Man amewachana wasanii wanaoogopa kufunga ndoa kwa madai ya kushuka kimuziki ambapo si kweli.

Mwanamuziki huyo amefanikiwa kufunga ndoa mkoani Morogoro wiki tatu zilizopita na mpenzi wake wa siku nyingi.

Tunda Man amesema kuwa wasanii wanaoongopa kufunga ndoa wakihofia kushuka kwa muziki, hawana hofu ya Mungu kwani kupanda na kushuka ni mipango ya Mungu na wapo kina Mr. Blue wamefunga ndoa na bado wanafanya vizuri kimuziki hadi sasa.

Pia Tunda Man amewapongeza wasanii waliofunga ndoa hivi karibuni akiwemo Nyandu Tozi, Mwana Fa, Mabeste na wengine.

Wasanii ambao wamefunga ndoa mwaka huu ni Mwana Fa, Tunda Man, Mabeste, Nyandu Tozi pamoja na mwanadada Khadijanito.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *