Kumekuwa na malalamiko na sintofahamu ya muda mrefu juu ya muziki upi ni bora zaidi baina ya muziki wa zamani na muziki wa sasa.

Mvutano huo wa mitazamo mara nyingi umekues ukipelekea mashabiki kuchagua vigezo vya kupima ubora wa muziki na hili limekuwa tatizo kubwa kwani mashabiki wengi sio wataalamu wa muziki.

Staa wa Hip Hop kutoka kundi la WEUSI, Nick wa Pili amedai kuw amkanganyiko huo unatokana na utofauti wa vigezo vya kupimia muziki ambapo kwa miaka ya siku hizi vigezo vimekuwa ni VIEWS za Youtube, FOLLOWERS kwenye mitandao ya kijamii na LIKES na COMMENTS za mashabiki.

Je, muziki wa zamani ambao ulikuwa unachezwa kukiwa hakuna vitu hivyo ulikuwa unapimwa kwa vitu gani? Ni suala la kuwatafuta wakongwe na kuwahoji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *