Rais wa Marekani Donald Trump amemshukuru Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuagiza kuondoka kwa wafanyakazi 755 kutoka kwenye afisi za kibalozi za taifa hilo nchini Urusi.

kiongozi huyo amesema angependa kumshukuru sana kiongozi huyo wa Marekani kwa kuisaidia Marekani kuokoa fedha.

Uchunguzi unafanyika nchini Marekani kubaini iwapo kulikuwa na ushirikiano kati ya maafisa wa kampeni wa Trump na Urusi, inayodaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

Mwishoni mwa mwezi Julai, Rais Putin alisema wafanyakazi 755 wangelazimishwa kuondoka kutoka afisi za kibalozi za Marekani nchini Urusi, akilipiza kisasi hatua ya Marekani kuiwekea Moscow vikwazo zaidi.

Wengi wa wafanyakazi hao ni waajiria wa kutoka Urusi, ikiwa na maana kwamba watu ambao watalazimishwa kuondoka nchini humo hawafiki 755.

Alisema watatakiwa kuondoka kufikia tarehe 1 Septemba, na kufikisha idadi ya wafanyakazi katika afisi za kibalozi wa Marekani hadi 455, sawa na wafanyakazi wa kibalozi wa Urusi walio Washington.

Wafanyakazi katika ubalozi wa Marekani mjini Moscow, pamoja na afisi za kibalozi katika miji ya Ekaterinburg, Vladivostok na St Petersburg wameathiriwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *