Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imezindua huduma mpya za mawasiliano kwa kutumia teknolojia ya 4G LTE.

Huduma hiyo itawezesha wakazi wa eneo hilo, kuwasiliana kwa ufanisi na gharama nafuu zaidi na kufanikisha shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba ameema kuwa Zanzibar inakuwa eneo la nane kupata huduma za 4G na lengo la TTCL ni ifikapo Desemba mwaka huu nchi nzima iwe imeunganishwa kwa huduma za TTCL za 4G LTE.

Amesema TTCL imeona vyema kuungana na Wazanzibari katika sherehe za Mapinduzi na kufuata nyazo za waasisi wa Mapinduzi kwa kuwapatia zawadi ya kutumia mawasiliano, ambayo itawezesha juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za kuwaletea wananchi wake maendeleo, kufanikiwa kwa wepesi zaidi.

Mikoa ambayo tayari imeunganishwa na 4G LTE kuwa ni Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza, Mbeya, Morogoro na Pwani.

Kindamba alisema menejimenti ya TTCL inahakikisha kuwa uzinduzi wa huduma ya 4G LTE mjini hapa, utakuwa ni mwanzo wa TTCL mpya, yenye huduma bora za kabla na baada kwa wateja, yenye huduma za uhakika wakati wote na mahali popote iwe ni nyumbani, sehemu za kazi, na hata kwenye vyombo vya usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Alisema kutokana na uhusiano mkubwa wa kijamii na kiuchumi kati ya visiwa vya Unguja na Pemba, pia aliahidi ndani ya muda mfupi eneo la Pemba kuunganishwa na huduma za 4G LTE ili eneo lote la Tanzania Visiwani lifaidi huduma hizo kwa ajili ya kukuza maendeleo na kupambana na umaskini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *