Klabu ya Yanga itawakosa wachezaji wake wanne kwenye mechi ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Welaita Ditcha ya Ethiopia baada ya kuoneshwa kadi zanjano kwenye michezo iliyopita.

Wachezaji hao ni pamoja na Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Said Juma Makapu na Kelvin Yondani.

Kwa mujibu wa sheria za CAF mchezaji yeyote akipata kadi mbili za njano kwenye mechi za kimataifa basi mchezo unaofuata hatoweza kushiriki kwa namna yeyote ile.

Yanga itahitajika kupata ushindi katika mchezo huo ili waweze kujikatia tiketi ya moja kwa moja kuingia katika hatua inayofuata ya makundi katika michuano hiyo ya kombe la shirikisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *