Kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi amekabidhiwa kiasi cha shilingi milioni baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwezi Februari.

Awali Tshishimbi alipaswa kukabidhiwa zawadi hiyo mapema lakini ilishindikana kutokana na klabu yake kuwa nje ya nchi katika mashindano ya kimataifa.

Tshishimbi amekabidhiwa tuzo hiyo na Wadhamini Wakuu wa Ligi, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania pamoja na King’amuzi cha Azam kutoka Azam Tv.

Tshishimbi alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwabwaga washindani wake, Emmanuel Okwi wa Simba na Pius Buswita wa Yanga, kufuatia kuisaidia timu yake kujikusanyia alama 12 huku akifunga mabao matatu na kutengeneza moja.

Okwi yeye alifunga mabao matatu na kuisaidia Simba kujikusanyia alama 10 huku ikienda sare mchezo mmoja na kushinda mitatu.

Buswita alifanikiwa kuifungia Yanga jumla ya mabao mawili pekee kwa mwezi huo Februari katika klabu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *