Mgombea urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican, Donard Trump amesema walinzi wa Bi Clinton wapokonywe silaha walizo nazo ndipo watu waone kitakachomtokea Bi Hillary Clinton.

Bwana Trump alikuwa akizungumza na wafuasi wake katika mkutano wa kampeni huko Miami ,akitetea hoja yake kwamba raia wa marekani zaidi wana haki ya kumiliki bunduki.

Hillary Clinton
Hillary Clinton

Anadai kuwa Bi Hillary Clinton anataka kuwaondolea sheria inayowapa haki hiyo.

Wafuasi wa Bi Clinton wanasema kauli hizo za Trump hazikubaliki kwani ni za kuchochea ghaisia.

Mwezi uliopita Trump aliwahimiza wafuasi wake wafanye kila kinachowezekana kumzuia Bi Clinton kuiondoa sheria hiyo matamshi ambayo wana Democratic waliyatafsiri kama uchochezi na vitisho vya kumtishia maisha mgombea wao Bi Clinton .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *