Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amelikashfua shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kwa kuliita baraza la kupiga gumzo.

Trump kupitia akaunti yake ya Twitter amesema shirika hilo linamsikitisha kwa madai kwamba badala ya kuwa shirika lenye hadhi kuu zaidi limekuwa kama baraza la watu kukusanyika na kupiga gumzo.

Kauli hiyo inafuatia baada ya jaribio lake la kutaka kupinga azimio lililokemea mpango wa Israel kuendelea kujenga makaazi yao katika ardhi ya Wapalestina kufeli.

Baraza la usalama la Umoja wa Matifa limesema kuwa Israel inakiuka sheria za kimataifa kwa kujenga katika ardhi ya Wapelestina.

Azimiio hilo lilipitishwa Ijumaa iliyopita huku Trump akitoa onyo kwamba mambo yatakuwa tofauti wakati atakaposhika rasmi hatamu za uongozi wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *