Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa huenda Marekani ikabadili msimamo wake kuhusu mpango wa makubaliano ya tabia nchi ya Paris.

Trump alijiondoa katika makubaliano hayo 2015 mwezi uliopita, akitaka kujadili upya kwa makubaliano hayo ili kutoiweka Marekani katika hatua isiyo na manufaa kwake kibiashara.

Kwa upande wa Rais wa Ufaransa Michael Macron amesema kuwa ni muhimu kuweka makubaliano hayo kando huku viongozi hao wawili wakizungumza vile watakavyofanya kazi kuhusu maswala kama vile kusitishwa kwa mapigano nchini Syria na ushirikiano wa kibiashara.

Pia amesema kuwa Trump ana ahadi za uchaguzi alizowapatia raia wa tafa lake na pia mimi nilikuwa na ahadi, je vitu hivi vinapaswa kuturudisha nyuma katika maswala yote?.

Macron na Trump baadaye walizungumza kuhusu juhudi za pamoja za mataifa hayo katika kukabiliana na ugaidi na hususan kundi la wapiganaji wa Islamic State nchini Syria na Iraq.

Macron amesema kuwa Ufaransa itaweka mikakati kadhaa ili kusaidia kuimarisha uthabiti katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *