Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa anaamini Barack Obama ndiye anahusika na maandamano dhidi ya uongozi wa Republican.

Trump amesema kuwa anafikiri Obama anahusika kwa sababu ni watu wake wanaohusika kwenye maandamano hayo ya kupinga uongozi wake.

Trump hakutoa ushahidi wowote kwa madai yake na Obama bado hajajibu lolote kuhusu suala hilo alilozungumza Trump.

Alipoulizwa kuhusu maandamano yanayohusu uhamiaji amesema kuwa ni wafuasi wa Obama waliohusika kuandamana.

Hayo yamejiri baada ya baadhi ya raia wa Marekani kuandamana na kupinga uongozi wa Trump ambao uliingia madaraka mapema mwaka huu.

Trump amekuwa hana mahusiano mazuri na mtangulizi wake Obama kutoka chama cha Democratic toka wakati wa kampeni za urais nchini humo mnamo mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *