Mgombea Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump amebadilisha mwelekeo wa kampeni zake na kujikita kwenye masuala ya uchumi baada ya wiki ngumu ya kuanza kampeni za uchaguzi.

Trump akiwa mjini Detroit ameahidi kuibua uchumi wa Marekani kwa mwendo wa kasi kwa kufuta kodi za mashirika endapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo mwezi Novemba.

Amesema nafasi nyingi za kazi zitatengenezwa kwa mabadiliko hayo ya mfumo wa kodi sanjari na makubaliano mapya ya mkataba wa kibiashara wa kanda ya Marekani ya Kaskazini.

Trump amesema kupunguza kodi ndio itakuwa kitovu cha mipango yake ya kukuza uchumi wa Marekani iwapo atashinda katika uchaguzi wa Novemba.

Katika hotuba yake kubwa ya sera za uchumi aliyoitoa mjini Detroit huku akikatishwa mara kwa mara na kelele za waandamanaji.

Trump amesema kiwango cha kodi kwa wafanyakazi kitakuwa kidogo mno hivyo kuzalishwa kwa mamilioni ya kazi kwani anataka kufungua ukurasa mpya kwa uchumi wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *