Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya uchaguzi wa rais nchini Marekani, Hillary Clinton na Donald Trump wanajitayarisha kwa wikiendi ya mwisho ya kampeni.

Bwana Trump atazuru majimbo matatu muhimu yakiwemo Florida, Carolina Kaskazini, na Nevada, wakati Bibi Clinton akifanya kampeni Florida.

Kura za maoni za karibuni kabisa, zinaonyesha kuwa mgombea wa Democratic Hillary Clinton bado anaongoza lakini yuko mbele kidogo tu ya mpinzani wake, Donald Trump.

Trump ametoa wito kwa wafuasi wake wasaidie kuzuia udanganyifu na ameonya kuwa kunaweza kutokea ulalamishi kwenye uchaguzi.

Na huko Ohio, jaji wa serikali kuu, ameionya kampeni ya Trump na ametoa amri kwa mshauri mmoja wa kampeni hiyo aache kuwatisha wapigaji kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *