Rais wa Marekani, Donald Trump amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa China Xi Jinping kuhusu kutambua sera ya “China Moja” ambapo ni elimu ya kidiplomasia, kwamba kuna serikali moja tu iitwayo China.

Trump alitilia shaka sera ya muda mrefu ya china, pale alipofanya mazungumzo na Rais wa Taiwan mwezi Desemba mwaka huu.

Hiyo ni mojawepo ya hatua kubwa mno ya kuvunja tamaduni ya muda mrefu ya kufuata taratibu ya uongozi, na kuchochea malalamiko rasmi kutoka kwa utawala wa China.

Mazungumzo hayo ya simu ni ya kwanza kati ya marais hao wawili tangu Trump alipoingia ofisini Januari 20, licha ya Rais Trump kuwapigia simu viongozi wa mataifa kadhaa duniani.

Viongozi hao wawili walialikana kuzuru mataifa yao, inasema taarifa hiyo, huku wakitarajia kuendeleza zaidi mazungumzo yao.

Taarifa kutoka Beijing zinasema kwwamba, China inampongeza Bw Trump kwa kutambua sera ya China Moja.

Mazungumzo hayo ya simu yalifuatia barua iliyotumwa na Trump kwa Rais Xi hapo jana hatua ya kwanza ya Trump kumfikia kiongozi huyo wa China.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *