Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa jeshi la Marekani liko tayari kuishambulia Korea Kaskazini wakati wowote.

Ameyasema wakati vita ya maneno kati ya nchi hizo ikizidi kushamili kuhusu mpango wa Korea Kaskazini kuendelea kufanya majaribio ya silaha za nyuklia.

“Suluhu ya kijeshi sasa ipo, imepangwa na iko tayari, Korea Kaskazini wakidhubutu kuchukua hatua isiyo ya busara basi itamgharimu Kim Jong-un” Trump ameandika kwenye Twitter.

Trump ameandika hivyo katika ukurasa wake wa Twitter mara baada ya kutishiwa kushambuliwa na Korea Kaskazini.

Vile vile, amesema kuwa Korea wasithubutu kutoa vitisho zaidi kwa Marekani kwani watajibiwa kwa moto wa ghadhabu ambao utaishangaza dunia.

Hata hivyo, siku za hivi karibuni kumekuwa na mgogoro mkubwa ambao umekuwa ukuzihusisha Marekani na Korea Kaskazini kuhusu suala zima la silaha za nyuklia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *