Rais wa Marekani, Donald Trump leo anatarajia kufanya ziara katika nchi ya Israel na Maeneo ya Wapalestina.

Atafika maeneo hayo akitokea Saudi Arabia, mshirika muhimu wa Marekani, ambako alitoa hotuba katika mkutano mkuu wa nchi za Kiarabu na Kiislamu.

Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel na Palestina katika kipindi cha siku mbili atakazokuwa eneo hilo.

Rais huyo amesema kupatikana kwa mkataba wa amani kati ya Waisraeli na Wapalestina yatakuwa mafanikio makubwa, lakini hakusema mkataba kama huo unafaa kuchukua mwelekeo gani.

Amesema angependa sana pande zote mbili ziamue kuhusu mkataba huo wa amana kwa mashauriano ya moja kwa moja.

Katika mkutano mkuu wa viongozi wa Kiislamu na Kiarabu mjini Rihadh siku ya Jumapili, Bw Trump

Trump pia alikariri tena kwamba anaamini amani kati ya Waisraeli na Wapalestina inaweza kupatikana.

Rais huyo wa Marekani amekuwa akichukuliwa sana kuwa muungaji mkono mkubwa wa Israel kuliko mtangulizi wake Barack Obama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *