Rais mpya wa Marekani, Donald Trump akiongea neno na rais Mstaafu Barrack Obama mara baada ya kukabidhiana madaraka kwenye sherehe iliyofanyika katika Ikulu ya White House mjini Washington siku ya Ijumaa.

Trump ameapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani baada ya kumshinda Bi Hillary Clinton kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana nchini Marekani.

Pia kwenye picha ya hapo juu inaonesha mke wa Trump, Melania Trump akiongea neno na mke wa Obama, Michelle Obama baada ya Bwana Trump kuapishwa kuwa rais wa taifa hilo lenye nguvu kubwa duniani.

Trump mwenye miaka 70 amepata upinzani kwenye kampeni zake baada ya kuwaongelea vibaya wahamiaji kwa kusema kuwa pindi atakapoingia madarakani hatopenda wahamiaji kuingia Marekani.

Rais huyo mpya wa Marekani baada ya kuapishwa ameanza kazi kwa kubadili sheria zilizowekwa na mtangulizi wake Barrack Obama ambapo amesema kuwa atahakikisha Marekani inakuza uchumi wake kwa biashara na mataifa ya nje.

Vile vile Trump amesema kuwa anatengeza ajira kwa vijana zaidi milioni 25 nchini Marekani baada ya kupewa mamlaka ya kutawala nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *