Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amesema biashara zake zitasimamiwa na kuendeshwa na wanawe wawili atakapochukua majukumu ya urais.

Wanawe hao ni Donald junior na Eric, ambao tayari wamekuwa wakitekeleza majukumu muhimu katika uendeshaji wa baadhi ya biashara.

Trump amesema atawakabidhi biashara hizo kabla yake kuapishwa na kwamba hakuna mikataba mipya ya kibiashara ambayo itaingiwa na kampuni zake kipindi ambacho atakuwa anahudumu kama rais.

Wakosoaji wa rais huyo mteule wanasema bado atakuwa hatarini ya kutokea kwa mgongano wa maslahi iwapo hataachilia umiliki wa biashara zake.

Bintiye mkubwa Ivanka, ambaye amekuwa akijihusisha sana katika shughuli zake hajatajwa popote, jambo ambalo limewafanya badhi kufikiria labda atapewa kazi rasmi katika serikali ya Trump.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *